PENZI LA KWELI NI SIRI AU HADHARANI?
(Is true love private or public affair?) Unafikiri mapenzi ya kweli ni ya siri au waziwazi? Katika mazingira ya mahusiano ya kimapenzi kawaida hisia za ndani zinamfanya au kumsukuma mtu kuonyesha na kutoa kilichopo ndani ya moyo wake, point ni kwamba unatumiaje nafasi hiyo? well kuna wengine imani yao ni kuweka mambo adharani ikiwa ni pamoja na kissing, kushikana hadharani, na mengineyo.
Ni kweli mapenzi hayawezi kuwa ya siri na wala hayafichiki lakini mashaka yetu ni kwa yale yanayofanywa hadharani.Inawezekana kwa wale wenzetu ni sawa lakinii kwa upande wetu au kwa asili yetu hilo limekaaje?
Is it okay? Lakini kuna msichana aliniambia tena strongly kwamba yeye hilo halimsumbui ili mradi tu watu wafahamu kwamba yule ni mali yake yeye "So Stay Away"
Is it okay? Lakini kuna msichana aliniambia tena strongly kwamba yeye hilo halimsumbui ili mradi tu watu wafahamu kwamba yule ni mali yake yeye "So Stay Away"
Utakuta Kuna wanaume baadhi huwa wana tabia ya kujionyesha kwa wenzao au kwa watu kwamba yeye ni mwanaume kamili kwa kufanya mambo hayo hadharani yeye hiyo haimsumbui kabisa kwamba anajivunjia heshima na ndio kwanza mkipita wote wawili mnafanya hivyo kwakweli kabisaa utaonekana kwa watu wanaowaangalia kuwa wewe msichana huna thamani yoyote, hujiheshimu, na wakati mnafanya wote wawili. Na ukitaka kuthibitisha hilo hata wakati wa haja ndogo mwanaume anaweza kujisaidia popote pale lakini si kwa msichana ni vigumu sana. kwahiyo unachotakiwa kuangalia msichana huo ndio utu wako? Na husijali kwamba tuko wawili. Maana mwenzako yuko kwenye show off!!
Kwa mimi sitapenda kujibu direct ila cha muhimu ni kujua mapenzi yenu wawili yanawahusu nini wengine? Na mnapokuwa kwenye raha zenu wanaofaidi ni nyie sasa ya nini watu wengine waone au kushuhudia? Mapenzi ni starehe ambayo huwezi kuilinganisha na kitu chochote duniani na unapokuwa kwenye idara hiyo akili yote inapotea. Kwahiyo ni vizuri sana mkaangalia sehemu ambayo nyie wote wawili mtakuwa huru na kuweza kufurahia mambo mnayoyafanya.
Ila Nitapenda kusikia kutoka kwako hivi kwelikweli mwanaume anayekupenda for real na ana hadhi yake anaweza kufanya hayo kwako hadharani? na je watu kama hao unawachukuliaje?
0 Response to "PENZI LA KWELI NI SIRI AU HADHARANI?"
Post a Comment