NIMECHOKA KUMSALITI MUME WANGU - Bongo Loves

NIMECHOKA KUMSALITI MUME WANGU

Niliolewa na mume wangu April 2010. Ingawa kwa mara ya kwanza sikuwa nampenda mume, lakini nilikuwa nazidi kuzeeka na sikuweza kumpata mwanaume yeyote wa dini yangu na kabila langu, wazazi wangu walinitambulisha kwa huyu mwanaume na kunilazimisha niolewe nae. Mara ya kwanza natoka nje ya ndoa ilikuwa bahati mbaya. Nilikutana na mpenzi wangu wa zamani na tukabadilishana Pins zetu za BlackBerry. Huwa tunachat mara zote na nikaanza kutoifurahia ndoa yangu kwahiyo nikamshawishi huyu ex wangu. Tukaanza kukutana na kuanza kufanya mapenzi. Baadae akahama kutoka huku mjini na kuhamia mji wa mbali na hatimae mahusiano yetu yakaishia hapo. Kutoka hapo nimekuwa na mahusiano na wanaume wengine wanne akiwemo mume wa rafiki yangu. Nina watoto wawili na mume wangu lakini siridhiki katika mapenzi. Mume wangu ni mpole na ananipenda, na nimetokea kumpenda lakini nashindwa kuacha mahusiano yangu ya nje ya ndoa. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mume wangu hajui chochote kinachoendelea. Simpi nafasi yoyote ile ya kuwa na wasiwasi na mimi. Nafuta sms zote kwenye simu yangu ingawa huwa hana tabia ya kuchungulia simu zangu. Nahakikisha hagundui chochote kwasababu nataka familia yetu isisambaratike. Hivi karibuni nimeongea na mchungaji wangu ambaye amenishauri niendelea kumwomba Mungu na kufunga lakini hii hainisaidii kwasababu bado naendelea kutoka nje ya ndoa. Najua natakiwa kuacha lakini sijui ni vipi. Tafadhali nisaidieni. USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "NIMECHOKA KUMSALITI MUME WANGU"

Post a Comment