NDOA BILA TENDO....MSADA JAMANI - Bongo Loves

NDOA BILA TENDO....MSADA JAMANI

Wapenzi salaam, Nina mkasa, au jambo ambalo linamsumbua dada yangu kwa kiasi kikubwa sana,nimeshare nanyi kwa kuwa najua kwenye wengi hakukosekani busara na majibu ya maswali magumu. Nina dada yangu mumewe anashindwa kumpa unyumba kwa miaka sita sasa, hata akijitahidi kukutana na mkewe anaishia njiani,yaani katikati inasinyaa, hii inatokana na nini, dada yangu kajaribu kila kitu hadi sasa anataka kuchukuwa maamuzi mazito, maana hamwoni muwewe kama anasumbuka na hilo kabisa,akimwongelesha hilo anakuwa mkali, na kukumbushia maugomvi ya zamani ili tu dada ajisikie vibaya. Mimi kaka mimi nimemshauri kama aliweza kukaa miaka yote sita asiachane na mumewe, kwani ana watoto nae nahisi watapata taabu kisaikolojia, dada yangu anampenda sana mumewe, coz hata akijaribu kucheat huwa hasikii raha wala nn,anamwazia mumewe tu,mwishowe anamwacha mpenzi na kurudi home kujituliza, hali hii imemfanya akose raha kabisa,japo kila kitu kiko fresh kimaisha,ukimwona akiwa na mumewe utadhani anafuraha hakuna dosari,ila muda mwingi ,ushauri wenu unaombwa.naomba wenye uzoefu na hata waliowahi kukubwa na tatizo hili wasaidie kutoa ushauri,pia wanaume ambao waliwahi kupatwa na tatizo hili mtoe ushauri tumsaidie mwenzetu.

0 Response to "NDOA BILA TENDO....MSADA JAMANI"

Post a Comment