Nchi ambayo wanaotoa mimba ni wengi zaidi ya wanaojifungua - Bongo Loves

Nchi ambayo wanaotoa mimba ni wengi zaidi ya wanaojifungua


Realistic looking baby dolls.Haki miliki ya pichaPAARISA
Image captionMradi wa mwanasesere uliwapa mwangaza vijana wadogo kujua umuhimu wa kuwajali watoto na kupunguza mimba zisizotarajiwa.

Msichana ambaye alitoa mimba mara tano ndani ya miaka miwili iliyopita.
"Huwa ninatumia kinga kila mara lakini wakati mwingine huwa tunasahau. Siwezi kuwa na mtoto kwa sasa, nko mwaka wangu wa mwisho wa masomo," msichana mdogo kutoka mji mkuu wa Nuuk, Greenland.
Na msichana huyo hayupo peke yake.
Tangu mwaka 2013, Watoto wapatao 700 wanazaliwa kila mwaka huku mimba 800 zinatolewa pia kila mwaka , kwa mujibu wa takwimu za serikali ya nchi hiyo. Lakini kwa nini Greenland kuwa idadi kubwa ya watu wanaotoa mimba ?
Woman walking with childrenHaki miliki ya pichaCHRISTIAN KLINDT SOELBECK
Image captionKatika mji mkuu wa Nuuk, wanafunzi wanajua kuwa kila jumatano ni 'siku ya utoaji mimba'

Kiwango kidogo cha unyanyapaa

Greenland ni kisiwa kikubwa duniani lakini chenye idadi ndogo ya watu, Takwimu ya mwezi Januari mwaka huu inasema kuwa Greenland ina idadi ya watu 55,992 peke yake .
Wanawake zaidi ya nusu ya wanaopata ujauzito huwa wanautoa. Na hii inafanya idadi ya mimba zinazotolewa kuwa 30 kwa kila wanawake 1000.
Ukilinganisha na Denmark ambapo idadi ya mimba zinazotolewa ni 12 kwa kila wanawake 1000, takwimu zinaainisha.
Hali ngumu ya kiuchumi ,makazi duni pamoja na ukosefu wa elimu vinaweza kuchangia idadi ya utoaji mimba kuwa kubwa.
Lakini hawaelezi kwa nini idadi hiyo ni kubwa kiasi hicho wakati dawa za kujikinga kupata mimba ni bure na zinapatikana kiurahisi.
Katika nchi nyingi, hata maeneo ambayo kutoa mimba inaruhusiwa na bure, kuna unyanyapaa kuhusiana na uamuzi huo wa utoaji mimba.
Greenland, baadhi ya wanawake hawana wasiwasi au hofu juu ya utoaji mimba, hawaoni kama ni jambo baya kutoa mimba na jambo la aibu kulizungumzia au kulifanya.
People standing, Greenlandic and Danish flagsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPamoja na kuwa Greenland imefadhiliwa na Denmark kwa kiasi kikubwa lakini kisiwa hicho kina bunge lake.

Siku ya kutoa mimba

Lakini kwa nini kuna idadi kubwa ya mimba zisizohitajika?
" Rafiki zangu wengi waliwahi kutoa mimba. Mama yangu aliwahi kutoa mimba tatu kabla hajanizaa mimi na kaka yangu ingawa huwa hazungumzii," alisema Piia.
"Wanafunzi katika mji wa Nuuk huwa wanaweza kwenda kiliniki kwa ajili ya afya ya uzazi kila jumatano na huwa wanaiita siku hiyo kama siku ya kutoa mimba" alisema Dr.Turi Hermannsdottir mtafiti kutoka Denmark.
"Mjadala uliopo Greenland kuhusu utoaji wa mimba kuwa jambo ambalo ni kinyume cha maadili na hata ngono kabla ya ndoa au kupata mimba bila kutarajiwa si jambo sahihi ."
Intra Uterine Device (IUD) and birth control pillsHaki miliki ya pichaMEDIA FOR MEDICAL
Image captionGreenland inatoa bure dawa za uzazi wa mpango lakini wanawake wengi hawazitumii

Dawa za bure za uzazi wa mpango

"Dawa za uzazi wa mpango ni bure na rahisi kupatikana lakini rafiki zangu wengi huwa hawazitumii," alisema Piia.
Stine Brenoe ni mtaalamu wa afya ya uzazi katika kisiwa hicho Greenland ambaye amekuwa anafanya utafiti kuhusu utoaji mimba kwa miaka mingi.
"Karibu asilimia 50 ya wanawake ambao nimewahoji walisema kwamba wana ufahamu kuhusu dawa za uzazi wa mpango lakini zaidi ya asilimia 85 hawazitumii dawa hizo kwa usahihi au hawazitumii kabisa.,"
mtaalamu alieleza.
Mimba zisizohitajika huwa zinapatikana kutokana na utumiaji wa pombe kwa kiwango kikubwa." Wanaume kwa wanawake huwa wanasahau kutumia kinga kama wako kwenye ushawishi"

Ushawishi

Kwa mujibu wa utafiti wake Hermannsdottir , alisema kuwa kuna sababu tatu zinazopelekea wanawake kutotumia kinga Greenland.
"Sababu ya kwanza ni wanawake ambao wanataka watoto , ya pili wanawake wenye tamaa na ambao wanaadhirika na pombe pamoja na vurugu huwa wana wanasahau kutumia dawa na mwisho mpenzi wake(mwanaume ) kukataa kuvaa kondomu.."
Tools for surgical abortionHaki miliki ya pichaSEAN GALLUP
Image captionUtoaji mimba uliruhusiwa Juni 12, 1975

Unyanyasaji wa kijinsia

Mwanamke anaweza kukubali kutoa mimba kama mimba hiyo ameipata baada ya kubakwa au msichana anakuwa hataki kumleta mtoto duniani akateseka.
"Kutoa mimba inawezekana kuwa ndio suluhisho zuri kwa watoto ambao hawahitajiki," alisema daktari Mosgaard, daktari wa wilaya moja iliyoko katika mji mdogo kusini mwa Greenland.
Unyanyasaji ni suala ambalo linachukuliwa kuwa la kiafya. Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 alishuhudia mama yake akiwa anapigwa na kufanyiwa fujo.
Mara nyingi watoto wamekuwa wakiathirika na unyanyasaji ambao wanashuhudia au kufanyiwa.
Moja ya tatu ya wakazi wa Greenland walifanyiwa unyanyasaji wakiwa watoto
Ditte Solbeck, afisa wa serikali alisema mipango iliyopo ya kupambana na unyanyasaji wa kingono kupitia televisheni .
Ilulissat, Greenland.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ufahamu mdogo kuhusu kinga

Licha ya kuwa kinga ni bure na rahisi kupatikana, hii haimaanishi kuwa wanatumia.
Niligundua kuwa sijanywa dawa ya kujikinga na mimba baada ya mwezi, sidhani kama kila mtu huwa anajua namna ya kujikinga na mimba ," Piia aliiambia BBC.
"Mama yangu hakuwahi kuongea na mimi kuhusu afya ya uzazi , nmejua nikiwa shuleni na kutoka kwa marafiki zangu," alisema.
Familia huwa wanakwepa kuongea kuhusu ngono au afya ya uzazi kwa kuona kuwa ni jambo gumu kuzungumza , utafiti uliofanywa na jarida la kimataifa la 'Circumpolar health' limeandika.
Local woman drinking and smoking in a barHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Idadi kubwa ya watu wanaojiua duniani

Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya utoaji mimba, Greenland ni eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu wanaojiua wenyewe.
Idadi ya watu 83 wanaojiua kwa kila watu 1000 kila mwaka kwa mujibu wa utafiti wa jarida la kimataifa la 'Circumpolar health'.
"Kuwa kijana katika eneo hili la Greenland ni ngumu kwa sababu utafiti unaonyesha kuwa vijana zaidi ya nusu huwa wanafanya jaribio la kujiua au wanajiua.
Karibu kila mtu anajua mtu ambaye alijiua.
Vilevile mfumo wa masiha wa kisasa, utumiaji wa pombe kupita kiasi na unyanyasaji wa kingono," alisema mwanasaikolojia mmoja nchini humo.
Women playing footballHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMoja ya tatu ya watu wazima wa Greenland wamewahi kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia , mamlaka imeeleza

Uhuru wa kutoa mimba kwa kila mtu

Greenland imeshauriwa kuweka gharama kwa kila mimba itakayotolewa ili idadi ya wanaotoa mimba ipungue.
Huku wengine wakikosoa kuwa wanawake kutoa mimba mara kwa mara haina uhusiano wowote kuwa kutoa mimba ni rahisi na bure.
"Ninapingana kabisa na uamuzi huo maana wanaweza kwenda kutafuta sehemu ambayo wanaweza kutoa mimba kwa gharama nafuu , jambo ambalo ni hatari," alipinga mtaalamu mwingine wa afya.
Baby dollsHaki miliki ya pichaPAARISA

Mradi wa mwanasesere


Serikali imeanzisha mradi unaoitwa "Doll Project" wakishirikiana na shule , wakilenga kuwaelewesha umuhimu wa kijana kuwa na mtoto katika umri mdogo.
Mradi huo umelenga kupunguza idadi ya vijana wanaopata mimba katika umri mdogo, kupunguza magonjwa ya zinaaa na kuwahamasisha watu kutumia njia za mpango wa uzazi.
Wavulana na wasichana wanapewa madoli ili wahisi kuwa ni watoto.
Njia hiyo imeleta mabadiliko na kuwafanya wanafunzi wenye umri kati ya 13 mpaka 18 kujua majukumu ya kuwa na mtoto yakoje.
Bila ya umri wa wanawake kuzingatiwa , wazo la wanawake kutoa mimba tu kuchukuliwa kuwa jambo rahisi si vizuri.
"Wanawake wengi huwa wanafikiria kuwa kutoa mimba ni maamuzi magumu na huwa wanachukua muda kufikiria kuchukua hatua hiyo kama wana uhakika au la.
Sijawahi kukutana na mwanamke ambaye hajali kuhusu kutoa mimba, ni jambo ambalo wanawake huwa wanaamua kukaa kimya au wanataka kujilinda ingawa wahudumu wa afya huwa wanakuwa na fikra tofauti.
Kuhukumiwa kwa wanawake wengi ndio kunasababisha matokeo haya", alisema Lars Pedersen mtafiti.
Aliongeza kwa kusema kuwa kuna tatizo la lugha ,wagonjwa wengi wanaenda katika hospitali ambazo wanapata changamoto ya lugha ya Denmark ndio inatumika.
Anadhani kuwa matatizo ya Greenland hayawezi kutatuliwa na wageni.
"Tunapaswa kufikiria tena namna ya kutatua matatizo yetu kulingana na mazingira yetu na changamoto zinazopelekea kuwepo kwa mimba zisizotarajiwa."


USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

0 Response to "Nchi ambayo wanaotoa mimba ni wengi zaidi ya wanaojifungua "

Post a Comment