Facebook: Kwanini akaunti bilioni 3 za watumiaji wa Facebook zimefungiwa? - Bongo Loves

Facebook: Kwanini akaunti bilioni 3 za watumiaji wa Facebook zimefungiwa?


Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.
Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki - idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.
Zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

    Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.
    Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

    "Sidhani suluhisho ni kuvunjilia mbali kampuni kwasababu tunashughulikia [tatizo hilo]," alisema.
    "Ufanisi wa kampuni hii umetuwezesha kufadhili mpango huu kwa kiwango kikubwa. Kiwango cha fedha tunazotumia kuimarisha usalama wa mtandao wetu ni kikubwa kuliko ''mapato ya mwaka mzima'' ya mtandao wa Twiter.

    Akaunti Bandia

    Facebook imesema kumekuwa na ongezeko la akaunti bandia kwasababu "wahalifu" wamekuwa wakitumia mfumo maalum kuzifungua.
    Lakini ikaongeza kuwa ilifanikiwa kuzigundua na kuzifuta zote katika kipindi cha dakika moja, kabla wapate nafasi ya kuzitumia kufanya "uhalifu ".
    Mtando huo wa kijamii pia utaripoti ni posti zilizotolewa kwa kuuza "bidhaa ambazo zimedhibitiwa"kama vile bunduki na dawa.
    Ilisema kuwa iliwachukilia hatua watumiaji milioni moja wa mtandao huo kwa kuuza bunduki katika miezi hiyo sita kipindi ambacho ilichukua kuaanda ripoti hiyo.
    Ripoti hiyo pia ilikadiria idadi ya ujumbe, kama zile zinazoangazia unyanyasaji watoto, ghasia na propaganda kuhusu ugaidii,zinazowafikia wateja wake.
    Kwa ujumla, karibu ya 5% ya watumiaji wa mtandao huo wanafanya hivyo kupitia akaunti feki.
    Uchunguzi huo ulibaini ni mara ngapi posti 10,000 zilizo na ujumbe huo zilionekana kwenye 

    Rufaa

    Kwa mara ya kwanza, ripoti hiyo ilifichua kuwa kati ya mwezi Januari na Machi 2019 zaidi ya watumiaji milioni moja wa mtandao huo walikata rufaa baada ya akaunti zao kufungiwa kwa kuposti ujumbe uliyo na ''kauli za chuki".
    Karibu watumiaji 150,000 walifunguliwa akaunti zao baada ya kubainika kuwa hawakukiuka sheria kipindi hicho.
    Facebook imesema ripoti hiyo imeangazia masuala hayo ili kuendesha huduma zake kwa njia ya uwazi na uwajibikaji ili kuufanya mtandao huo kuwa ''salama kwa wateja wake".
    :



       KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

      0 Response to "Facebook: Kwanini akaunti bilioni 3 za watumiaji wa Facebook zimefungiwa?"

      Post a Comment