Vijana wa kiume jueni hili kabla ya kuoa
VIJAN WA KIUME..!
KABLA HAUJAFIKIA UAMUZI WA KUOA NI VIZUR UKIFAHAMU NA KUFANYA YAFUATAYO 👇1.UWE UMEACHA MAMBO YA UVULANA.
🔹Ndoa ni kwa ajili ya watu waliokuwa na utimamu wa akili, hivyo hakikisha umeshaacha mambo ya kitoto/uvulana na umekuwa kiasi cha kustahiri kuitwa Kichwa cha familia, mume wa mtu na baba wa watoto.
2.JITENGE NA PUNGUZA MAZOEA MABAYA NA WASICHANA.
🔹Kuna watu wamezoea kuwa karibu sana na wadada kiasi kwamba hauwezi kutofautisha kama ni marafiki zake wa kawaida au wapo kwenye mahusiano.
🔹Sasa kama unataka kufanya Maamuzi ya kuoa INAKUBIDI kuweka mipaka kati yako na wadada, pia anza kujiheshimu acha kujiachia mpaka unapitiliza.
🔹Sina maana uache kabisa kuongea nao, ila weka mipaka, mf hauwezi ukawa una' hug' wadada ovyo, mara mnachat mpka saa 6 - 7 usiku na ukaribu uliopitiliza, Sasa unatakiwa kujiandaa kumfanyia mambo hayo mtu mmoja TU ambaye unataka awe mwenzi wako.
3.JIZOESHE KUJITEGEMEA KIAKILI.
🔹Mwanaume ni kichwa cha familia (Waefeso 5 :23), kichwa maana yake ni mtu mwenye uwezo wa kufanya MAAMUZI, kichwa ina maana ya kuwa kiongozi.
🔹Hivyo anza kutumia akili yako vizuri kutatua changamoto unazokutana nazo. Kama ulizoea kila unapopata tatizo ni lazima uombe ushauri kwa marafiki zako basi ACHA tabia hiyo na jizoeshe kufanya Maamuzi binafsi.
🔹Maana unaenda kuwa mtu wa kutegemewa na mke na watoto wako Katika changamoto mnazokutana nazo, sasa ukizoea kuomba ushauri mara kwa mara utakuwa SIRI za ndoa yako zote unawapa watu.
🔹Anza kuomba Mungu akuandae kuwa kichwa cha familia yako kwa kukupa HEKIMA na UFAHAMU.
4.JIANDAE KIUCHUMI.
🔹Sifa kubwa ya mwanaume ni kuwa na uwezo wa kujihudumia kiuchumi na kuhudumia pia watu wa karibu yake. Kuna wengine husema 'heshima ya mwanaume ni Kazi', nami pia naungana na kauli hiyo.
🔹Hakuna kiwango maalumu cha kujiandaa kiuchumi maana kila mtu ana kiwango chake binafsi, Lakini cha umuhimu ni kuwa na uwezo angalau wa kujihudumia na kuhudumia familia yako Katika mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, Mavazi, matibabu nk.
🔹Usitegemee mke Katika hili , hili ni JUKUMU lako la msingi na heshima yako pia. Maisha ni kusaidiana lakin hii haiondoi wajibu wako. Wengine mpaka mahari wanataka walipiwe na wachumba zao.. Aisee JIANDAE /JIPANGE.
🔹Acha zile stori za kina babu za kusema nilikuwa na mkeka TU na kitanda cha kamba wakati namuoa bibi yako, Dunia ya sasa sio ile ya miaka ya 70' na 80 ' kama una mawazo hayo UTASUBIRI sana labda uoe bibi na si wasichana hawa wa sasa.
4.JIANDAE KUBEBA MAJUKUMU.
🔹Ndoa ni uwajibikaji na si sehemu ya ku' relax, unapoingia kwenye ndoa kama mwanaume unatakiwa kufahamu kuwa kuna familia kama 3 zinakutegemea.
🔹Baada ya kuoa unatakiwa kuwa msaada kwa familia uliyotoka, familia ya mwanamke na familia yako ya sasa (mke na watoto).
🔹 Hivyo unapaswa kujiandaa KIAKILI na KIUCHUMI kukabiliana na majukumu hayo. .....acha mawazo hasi ya kutaka kutafuta mwanamke mwenye mshahara ...ukidhani kuwa utaumiliki hilo sahau jishughulishe bado mapema...usimame ww km wewe
5.WEWE NDIO TASWIRA YA FAMILIA YAKO.
🔹Familia utakayo kuwa nayo inategemea na vile wewe ulivyo, mke na watoto wako wata 'copy na ku paste' tabia zako na msimamo wako.
🔹Ni muhimu kuanza kujiandaa kitabia, mtazamo na misimamo yako ya Maisha sasa na UANZE kuisimamia ili utakapompata mwanamke ambaye unataka kuwa naye AKUFAHAMU mapema kuwa wewe ni mtu wa aina gani na aanze Kuishi sawasawa na misimamo hiyo na kama HAWEZI basi mjue mapema kurekebisha baadhi ya misimamo hiyo au utafute yule anayeendana na wewe.
6.UWE NA MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU.
🔹Hii nimeitaja karibu na mwisho lakini si ya mwisho. Mwanaume anayemfahamu Mungu vizuri ni KIELELEZO kizuri kwa familia yake.
🔹Mungu humwangalia mwanaume kwanza kwenye familia kabla ya kumwangalia mwanamke, maana hata Katika uumbaji mwanaume ndio aliyeumbwa kwanza. 1 Timotheo 2 :23
🔹Mungu hutoa MAAGIZO ya familia kwa mwanaume kwanza na si kwa mwanamke, hata Katika bustani ya Edeni Mungu alimpa MAAGIZO Adamu na si Hawa. Mwanzo 2 :16
Itaendelea.........
0 Response to "Vijana wa kiume jueni hili kabla ya kuoa"
Post a Comment