Tafakari kwa Binti kabla ya kuolewa - Bongo Loves

Tafakari kwa Binti kabla ya kuolewa


Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi. Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku. Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele. Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.
Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye #HARUSI yake wamchangie.
Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;
=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?
=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)
=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?
=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?
*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?
*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?
*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?
*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?
*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.
*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo. Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.
Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo. Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.

0 Response to "Tafakari kwa Binti kabla ya kuolewa"

Post a Comment