Sababu 20 za kuoa/kuolewa na kuishi maisha ya furaha baada ya ndoa!
Je ulishajiuliza kua utaoa / kuolewa? Yafuatayo ni mambo 20 ya kuoa au kuolewa na kuwa na maisha ya furaha baada ya ndoa!
Ndoa zilipaswa ziwe zinafungwa Mbinguni.Lakini kwa kiwango kikubwa cha utoaji talaka, utabaki kujiuliza kama kweli hii ndoa ina manufaa au uachane nayo tu!
[Soma: Sababu kubwa 20 za talaka ambazo wanandoa wengi huzipitia!]
Kwa kufikiria kuhusu ndoa, na wazo la kuishi pammoja ni kitu kirahisi sana.
Najua unaweza ukashangaa na kujiuliza kwa nini ujifunge kwa kuwa na mtu mmoja maisha yako yote.
Kupitia ndoa, huibuka masuala ya uwajibikaji, ubishi / mabishano na changamoto nyingi zaidi za kimaisha - kama hamtakuwa makini.
Na kuna kitu fulani kuhusu ndoa kinacho fanya ndoa iwe jambo ambalo ni serious.
Ni kama vile unatakiwa
kuwa mtu mpya kwa usiku mmoja tu.
Lakini kwa upande mwigine, ndoa ina mambo yake mengi mazuri ya kuyaenzi pia.
Sababu kubwa za kuingia katika ndoa
Kama haupo tayari kuoa / kuolewa, inamaanisha haupo tayari kuingia katika ndoa. Na hii hali ni rahisi sana kuimudu.
[Soma: Ni umri upi sahihi sana wa kuoa / kuolewa?]
Ulivyokuwa / unapokuwa chuoni, unajua inakupasa wewe usome sana ili uweze kutoka na viwango vizuri vya ufaulu.
Na kama haukuwa tayari kufanya test kubwa za chuo, ulikua uki hairisha(post-pone) na utafanya siku nyingine. Kwa sababu ulijua hautafaulu, sasa kwanini ujiangaishe na test, Si ndiyo?
Na hii ni sawa na kwenye ndoa pia. Kama haujajiandaa kimwili na kisaikolojia kuingia katika ndoa, ni vizuri ukasubiri - muda bado upo, tafuta muda uliokuwa tayari.
Kumbuka maisha yana hatua. Unaweza ukasukumwa kuingia kwenye hatua fulani, lakini kwa sababu hukujiandaa kuingia katika hiyo hatua, hauta furahia hiyo stage!.
Na kama shuleni, chuoni, katika uhusiao wako wa kwanza, katika kazi yako ya kwanza, na wakati mwingine wowote unapokuwa kwenye jambo jipya, ndoa nayo ni hatua muhimu ambayo inabadilisha sana maisha ya mtu. Iwe nzuri, au mbaya, au vyovyote vile itakavyokuwa inategemea na jinsi ulivyokuwa umejiandaa kuipokea na kuimudu.
[Soma: Sababu za muhimu na za msingi za kuingia katika ndoa!]
Mara nyingi kama haupo tayari kuingia katika ndoa ni kwasababu haujampata mtu sahihi ambaye unahisi utahitaji kuwa naye maishani, au hauna kazi nzuri na ya uhakika, au unafikiri hauna pesa za kutosha, au unayapenda maisha yako jinsi yalivyo!.
Kama upo katika uhusiano wa muda mrefu kwa sasa na unajiuliza kwamba kweli unaweza kuuvaa huu wajibu mpya wa kuishi na mtu maisha yako yote kwa kitu kinachoitwa ndoa, zifuatazo ni sababu 20 za kuingia katika ndoa ambazo unapaswa uzizingatie. Kama utazitafakari kwa makini hizi sababu, utaelewa upande mzuri wa ndoa na utajua kama upo tayari au la!.
#1 Ni ahadi kubwa sana. Hakuna uthibitisho mkubwa wa upendo kama kumuuliza mpenzi wako kama mnataka muoane. Usiiangalie ndoa kama vile kofuli lisilokuwa na ufunguo. Ione ndoa kama mojawapo ya njia unayoweza kuweka ahadi yako kubwa kwa mpenzi wako kama ishara ya upendo.[Soma: Njia hadimu na ya kipekee ya kumuomba mpenzi wako muoane!]
#2 Una share maisha yako na mwingine. Sisi kama binadamu tumeumbwa kama kiumbe ambacho tunaweza kuingiliana na kushirikiana kwa pamoja katika jamii. Kuishi maisha ya peke yako inaweza ikaonekana kuwa nzuri kwa mwanzoni, lakini inafika wakati, kila mmoja wetu anajisikia kuhitaji mtu mwingine atakayekua anamuangalia, na kuwa na mtu mwingine ambaye unaweza ku shea nae furaha na matukio ya huzuni pia.
#3 Umesha enjoy sana maisha ya kuwa peke yako. Unakumbuka kipindi una miaka ya ujana na kipindi wewe upo single ulivyokua? Na sasa umebadilika, na hii itakuonesha kuwa maisha yamebadilika na umekuwa mtu wa tofauti, na unahitaji kuwa na mtu wa kushirikiana nae maishani, na si tu wakulala nae usiku.
#4 Hatua za maisha. Kama nilivyosema hapo awali, maisha ni mchezo wa hatua. Na kama umejiandaa kiakili na kimwili na kisaikolojia kuingia hatua nyingine, mawazo yako na akili yako yatakushawishi kuingia katika hatua hiyo inayofuata kwa kukuonesha faida zake. Na ndoa ni hatua muhimu sana katika maisha. Kama kweli unampenda mtu, jitwike hilijukumu. Utajipatia uzoefu mpya wa maisha ambao haukuuzoea na inaweza kukusaidia kuendeleza maisha.[Soma: Hatua 9 za mmahusiano ambazo kila wapenzi lazima waipitie!]
#5 Utamaduni. Ndoa ni utamaduni unaopenda kueleza majira. Na kama tulivyojiwekea utaratibu wa kuamini kuna wakati utafikia muda fulani ufanye kitu fulani - vivyo hivyo katika ndoa ina muda wake, na ndoa ni utamaduni uliozoeleka ya kwamba kama wawili wanapendana sharti waoane.
#6 Umezama kweli katika dimbwi la Upendo(Mapenzi). Umeshakuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu mmoja kwa muda mrefu na bado mnazidi kuwa nafuraha kilakukichwa? Kama ndiyo Upo tayari kuingia katika ndoa kuliko ulivyofikiri.[Soma:Sababu kubwa iliyojificha ya kwanini hauyapati mapenzi ya kweli!]
#7 Ndoa ni sapoti kubwa sana kwako. Unapokuwa katika wakati mgumu sana katika maisha unakumhbuka kuwa una mpenzi wako ambaye mnashirikiana katika mazuri na mabaya itakusaidia kurahisisha ugumu wa tatizo na mwishowe kulipatia ufumbuzi.
#8 Inahamasisha(Motivation). Ile tu kujua kuwa una mtu ambaye anakujali na kukuthamini kwa kila jambo unalofanya na kupitia, inakutia moyo na unakuwa na hari mpya ya kufanya kazi kwa bidii ili uweze kufikia malengo yako ya kuwa na maisha mazuri na mkeo. Kama kweli unampenda uliyemuoa, utapata hamasa ya kufanya kazi ili wote muwe na maisha mazuri.
#9 Ni Hadhi uhusiano wenu. Umekuwa na uhusiano na mwenzako kwa miaka mingi, Lakini uhusiano na ndoa ni vitu viwili tofauti japo vinategemeana. Mahusiano ya wawili kama hamjaoana huchukuliwa kama mahusiano ya kawaida. Na kama kweli unampenda mpenzi wako kwa nini msiupandishe uhusiano wenu hadhi na kuwa katika hadhi ya juu ya ndoa?[Soma:Kwanini kweli kama unampenda mtu - Unatakiwa usimuache!]
#10 Ni desturi ya Jamii. Ndoa ni jambo linalokubalika na jamii na hupendewa na kila mtu katika jamii kwa watu wa rika zote. Kwa hyo kama wote mnafanya kazi na mnaishi vizuri na jamii inayowazunguka na jamii inautambua uhusiano wenu, kilichobaki ni nyie kuoana tu. Inaweza isieleweke lakini ndoa kwa wapendanao ni jambo la kidesturi na sio jambo linaweza kukataliwa.
yyyyyyyyyyyyyyyy
0 Response to "Sababu 20 za kuoa/kuolewa na kuishi maisha ya furaha baada ya ndoa!"
Post a Comment