NINI CHA KUFANYA X WA MPENZI WAKO ANAPOKUSUMBUA
Tumekuwa tukisikia ama kupitia kwenye mahusiano yanayohusisha vurugu na utomvu wa nidhamu wa wapenzi wa zamani, ambao hawako tayari kumwacha mpenzi wako. Labda anafikiri kuna uwezekano wanaweza kurudiana ama anataka kukukwaza wewe mpenzi wa sasa kwenye mahusiano yenu kwa sababu ya wivu uliopitiliza. kwa sababu yoyote ile, Ni vigumu kuishi maisha ya furaha, ukiwa katika mahusiano mapya na wakati huohuo mpenzi ama wapenzi wake wa zamani wanamfuatilia mpenzi wako ni jambo gumu na la kukera.
Lakini kuna jambo moja, tunatakiwa kukumbuka kwamba "wazimu" wa mpenzi wa zamani unasababishwa na kupitia katika wakati mgumu (emotion), na yeye ni binadamu pia lazima apitie hilo, ila anajaribu kutatua wakati wake mgumu kwa njia zisizo faa. Kufanya mambo yaende vizuri, unatakiwa wewe kuwa na busara. Kama unataka akuache wewe na mpenzi wako muishi maisha yenu kwa roho safi, kuna mambo unatakiwa kuyafanya;
Jaribu kuchukua nafasi yake
Najua hii ni ngumu kwasababu huyu ni mwanamke ama mwanaume anaekusumbua, lakini kwa muda mfupi jifikirie ingekuwa ni wewe ungejisikiaje. Hebu fikiria anajisikiaje: Ni moja kwa moja anafanya hivi kwasababu ameumia moyoni mwake na hakuwa tayari kuachana na mpenzi wake. Ndiyo anajaribu kutatua hili kwa njia isiyo sahihi , na ndiyo si mtu mzuri kwako, lakini kama mwanadamu unatakiwa kuwa mtu mwema kwake. Amekwazika ndiyo sababu ya konyesha tabia zisizo za kawaida. Jifikirie utajisikiaje baada ya kuachana na mpenzi wako, na kumuona mpezi wako na mpenzi mwingine na wewe bado unampenda. Inaumiza na hiyo inaweza kuwa ni sababu ya yeye kuwa na tabia hizo.
Jaribu kumkwepa
Kabla ya kufanya lolote, jaribu kadiri ya uwezo wako kumkwepa. Wakati mwingine, kukwepa mtu anaejaribu kukukwaza ama kukukasirisha ni njia nzuri ama kutatua tatizo. Kwa kufanya hivi unamuonyesha hujali, na una mambo muhimu ya kufanya zaidi ya kumfikiria yeye. Jaribu kuishi kama hakuna lolote linaloendelea na endelea na maisha yako ya kila siku. usipokee simu zako wala kujibu meseji zake kwasababu huna la kujadili na yeye. Kama ataendelea kukusumbua ni vizuti kumblock kwenye mitandao ya jamii ama simu. Epuka kuwa karibu na marafiki zake ama watu wake wa karibu. Epuka kuzumgumza habari zake wala kufuatilia habari zake. Kama ushauri huu haufanyi kazi endelea kusoma ushauri unaoendelea.
Zungumza na mwenza wako kuhusu hili
Kama utajaribu kuyafanya hayo hapo juu na bado ataendelea kukusumbua, unatakiwa kuzungumza na mwenzi wako kuhusu linaloendelea. Mueleze ni jinsi gani mpenzi wake wa zamani anavyokufanyia na mueleze kwamba unakwazika sana na vitendo vyake. Kuwa muwazi kwake na mueleze hili kama wapenzi, ili mlitafutie ufumbuzi kama wapenzi. Anatakiwa kufahamu unavyojisikia kutokana na matendo ya mpenzi wake wa zamani.
Epuka kuharibu mambo
Najua kuna wakati unajaribu kufanya vitendo vitakavyomfanya mpenzi wake wa zamani apate wivu ili asiwasumbue tena. Utataka kupost picha ukiwa mmekumbatiana, mnapigana mabusu kwenye mitandao ya kijamii ambayo una uhakika ataziona, na wakati mwingine unaweka status kama "Nakupenda sana, hana muda na wewe tena", usijaribu. Huku ni kujiweka madoa mwenyewe. Kufanya vitendo kama hivi, ni kumuongezea hasira na hujui at react vipi. Hili litafanya hali iwe mbaya zaidi. Jaribu kutumia busara zaidi na hekima.
Mwambie Mwenzi wako azungumze naye
Kama mambo yanaendelea kuwa mabaya na yamekushinda kabisa, zungumza na mwenzi wako na mwambie anatakiwa kuzungumza na mpenzi wake wa zamani, kabla wewe hujazungumza nae lolote. Hii ni kwasababu yeye ndiye aliyekuwa na mahusiano naye na sisi wewe. Mueleze jinsi unavyojisikia na asipolifanyia kazi litakuja kuathiri hadi mahusiano yenu. Mwambie azungumze naye na amueleze anatakiwa kuacha vitendo vyake anavyo kufanyia na amueleze aelewe.
Usijaribu kupigana naye
Usajaribu kutatua hili tatizo kwa mikono yako, Usipigane naye wala kupambana naye kwa maneno makali kwenye mitandao ya jamii. Hili halitakusaidia bali litafanya mambo yawe mabaya zaidi na litaongeza shid zaidi.
Zungumza naye kiutu uzima zaidi
Badala ya kupambana, jaribu kusuluhisha hili tatizo kiutu uzima zaidi. Muuliza kama mnaweza kuonana ili mzungumze,. Au mtumie meseji kwenye Face book, na ujumbe huo usiwe wa kumtisha, kumlaani ama kumuonya. Kuwa muwazi kwake na mueleze upendi mambo anayoyafanya, uko very happy kwenye mahusiano yako na na utafurahi kama ataendelea na maisha yake na kuachana na nyinyi. Kuwa mwenye busara na jaribu kuzungumza nae kwa upendo na hakikisha ujumbe kauelewa. Hili litasaidia kumfanya atambue kuwa anatakiwa kuacha upuuzi. Kumbuka hili ni suluhisho la mwisho kabisa kama umejaribu kila njia na ikashindikana. Tuepuke vita juu ya mahusiano kwasababu haina tija yoyote.
0 Response to "NINI CHA KUFANYA X WA MPENZI WAKO ANAPOKUSUMBUA"
Post a Comment