Mwanaume na Mwanamke wanaotaka 'kutoka' wote V.s Mwanaume na Mwanamke wanaotaka kuoana! - Bongo Loves

Mwanaume na Mwanamke wanaotaka 'kutoka' wote V.s Mwanaume na Mwanamke wanaotaka kuoana!

Image result for mahusiano

Wanawake huamua vipi kuwa wewe ni mwanaume anataka kutoka na wewe tu au wewe ni wa kumuoa? Hapa utajifunza tofauti ya kuwa date material na busband material

Hakuna aliye zaidi ya mwenzake - wote tulizaliwa sawa, na katika hatua fulani katika maisha , unaweza ukawa unahitaji kuwa mwanaume anayetaka u date naye, lakini baadae utahitaji kuwa mwanaume anayehitaji kuwa naye maishani.

Sasa ni nini kinachomfanya mwanaume avutie msichana mpaka aamue kutoka nae?

Wanawake wanampenda mwanaume ambaye anavutia - "simaanishi kisura". Kama mwanamke anahitaji mwanaume wa kutoka naye tu na si wa kuishi naye, anapenda kuwa na mwanaume ambaye anamfurahisha na kumvutia. Uchaguzi wake huwa popote pale ambapo ataona pana mfaa.
Waanaume ambaye wanawake hupenda waolewe nao na kushi miaka yote, ni wale wanaume wanaoweza kumfanya mwanamke ajisikie analindwa, ana amani, na mwenye material au sifa za kuwa mume!.

Kujua unachokitaka katika maisha yako
na kile unachokitazamia kita toa picha ya mwanamke ambaye utaishi nae baadae.[Soma: Mambo 15 ambayo mwanamke huangalia kabla hajaamua kuwa na mwanaume!]

Ni jinsi gani ya kuwa mwanaume anayependa kuishi naye?

Kuwa mwene kujiamini na usiyetabirika wakati mwingine. Wanawake hupenda mwanaume ambaye anawafurahisha na kuwafanya watabasamu muda wote, na kama unaweza kuyafanya hayo kwa mwanamke, atakuwa na furaha sana wewe kuwa nae. Tatizo wanaume wengi sana siku hizi hupenda kuigiza na kujikuta wapole sana kiasi kwamba wanaboa.
Wanawageuza wanawake kama bidhaa na kuwabusu hovyo wakidhani wataonekana noma sana. Badala yake, kwa wanawake hiki ni kitu kikubwa kinachoweza kushushia CV kwa mwanamke.[Soma: Makosa makubwa 7 wanaume huyafanya wanapokuwa kwenye mahusiano!]

Wanawake hupenda ku date "Wanaume Wa Ajabu" kipindi bado wakiwa wadogo au umri wa kati - wakati bado hawajajielewa vizuri. Na wao hujua kuwa uhusiano huo haufiki popote pale, kwa hiyo hujichagulia watu wa kuwafurahisha kwa muda mfupi - na kwenda kwa mwanaume ambaye anavutia kwa wakati huo, japo wanajua hawapo serious. Wanaume ambao hupenda tu ku date na sio kuwa katika mahusiano ambayo yapo serious hupenda kujua jinsi gani ya kuwa sukari ya warembo.[Soma: Njia 25 noma za kuwa Sukari ya Warembo!]

Wanaume ambao ni "Sukari ya Warembo" hujipenda wenyewe na huangalia maisha yao wenyewe, na pale mwanamke anapokuwa mbali nae - hana habari nae anatafura mwingine. [Soma: Sukari ya Warembo Vs. Good Boys - Wanawake huwapenda wanaume wa aina ipi?]

Hizi tabia mara nyingi sio za kuvutia wala hazileti heshima kwa mwanaume, lakini hazitoki kutoka sehemu mbaya au kwa watu wabaya - hutoka kwa watu ambao hufoji njia zao za kuishi katika maisha yao, na kama mtu atajipendekeza kwake - hiyo kwake poah tu. Na kama hatajipitisha - pia sawa tu!.
Fikiria wasifu fulani katika Movie, Mfano James Bond au Jason Statham katika Transporter. Wana hii tabia - wana mission zao katika sehemu mbalimbali katika dunia hii na huzifata mission zao bila ya kujali wengine wanafikiria nini - ilimradi tu katimiza wajibu wake, na hiki ndicho kitu kinachowafanya wavutie sana.

Mwanaume wa hivi anakuwa na options nyingi sana anapokutana na mwanamke. Hajawekeza sana kwa mtu mmoja, lakini kajiwekezea kwake binafsi. Anaweza ku date kwa muda mfupi lakini muda mwingi anafanya mambo yake. Namna wanawake wanavyompenda kwa yeye alivyo disminder ni uhalisia uliopo katika jamii. Kama wengine wanampenda , itakuwa kuna jambo linavutia kutoka kwake, kwa jinsi anavyofikiri na mitazamo yake.[Soma: Sababu 10 za kwanini wanawake wanaopenda ku date na wanaume wa ajabu 'Bad Boys'!]

Jinsi ya kuwa mwanaume wa kumuoa!

Hizo tabia tulizozisema hapo juu bado zinavvutia sana kwa wanawake, lakini kuwa mwanaume ambaye anapenda aishi nae miaka yote inahitaji mambo mengi ya ziada na ya utofauti mkubwa sana.
Haupendi kuwa mtu wa kutabirika na mwenye kuboa, lakini unatakiwa uwe salama na mwenye Kujilinda. Anahitaji kujua kama unaweza ukaijali familia, utatoa na kutimiza mahitaji yote, na utakuwa baba mzuri?. Iwe unataka kuwa na mtoto sasa, baadae au hautaki kabisa kuwa na mtoto, bado wewe kuonesha ishara za kuwa baba mzuri zitadhihirisha kuwa utakuwa mume mzuri pia.
Kuwa imara na mwenye maamuzi, lakini wakati huo huo, kwa hekima kubwa zamisha upend0o wako na uwapendao hasa familia yako na ndugu zako. Jijengee utu wa kuwa mtu muwajibikaji kwa matendo yako, na pia kuwa tayari kumuhusisha mwenzako katika maamuzi unayotaka kuyachukua.

[Soma: Mambo 9 Kutoka kwako Yanayodhihirisha ushakuwa Husband Material!]

Unapokuwa katika uhusiano sanasana unapokuwa bado mdogo / kijana, kuwa "msanii" inaonekana siyo kitu kibaya kabisa - ni jambo la kawaida. Lakini sasa unapofikia hatua ya kutaka kutulia na kuishi na mmoja, muishi wote mpaka muwe na watoto, mwanamke atayathamini sana hayo mafanikio. Kuwa na kazi nzuri ambayo itakusaidia wewe na mwenzako ni jambo la muhimu.
Hakuna mwanamke anayependa kuishi na mwanaume ambaye hana kazi - eti amlishe na kumpa mahitaji yote kama mtoto mdogo. Na hii ndo mana ni vizuri kujituma katika kazi yako ili ifanikiwe na iongezeke viwango kabla hata haujaamua kuishi na mwanamke wako.[Soma: Viwango 25 vitakavyo kufanya u fit kwenye maneno na majina yote mazuri!]

Unatakiwa kujua, maamuzi ya kuingia katika uhusiano ambao upo serious siyo jambo rahisi / jepesi, ujue ya kuwa mwanamke unayetaka kuishi nae , na yeye atayasikiliza mawazo ya wazazi wake pamoja na marafiki zake. Kama wewe ni mwanaume mwema, mchapakazi, mtulivu na mwenye hekima, Lazima uchukue point zote kutoka pande zote zinazomzunguka.

Waoneshe kuwa unaweza kumuhudumia mwanamke wako vizuri, na watampa baraka zote. Kama wale wanaomzunguka hawatakupenda, bora uachane na huo uhusiano maana mambo yanaweza kuwa mabaya baadae.Vinginevyo uwe mwangalifu na mbunifu ili uweze kuwashawishi wakuelewe.
[Soma:Je wewe ndiye aina ya mwanaume anayeweza kukutambulisha kwa mama yake?]

Ni kweli, haitakiwi uburuzwe inatakiwa uwe mwanaume wa kujitegemea, unayefata ndoto zako na matamanio yako, na unajituma ili uwee kuishi maisha ya ndoto zako. Tofauti tu ni kwamba kwa sasa unahitaji kuwa na ndoa na familia, na hizi zinatakiwa ziwe / viwe vipaumbele vikubwa katika maisha yako.

Sasa unatakiwa uwe vipi?

Kwa mtazamo wangu, mwanaume anatakiwa muda mwingi sana wa ujana wake autumie na kujituma na kuwekeza katika maendeleo binafsi na maendeleo ya familia yake ya baadae. Hii inamaanisha jifunze mengi ukiwa na umri mdogo na mambo hayo yakujenge ili uwe mtu mzuri baadae.
Unapo fika katikati ya miaka 26 - 29 ndiyo muda wa kukaa sasa na kuwaza mipango ya familia unayoihitaji, na ndiyo muda wa kutulia. Katika huu wakati unatakiwa sana uangalie mienendo yako na tabia zako wakati unaendelea kupigana kuzitimiza ndoto zako. Kama unataka kudate, hangaika ni jinsi gani unavyoweza kuvutia na kuwa na mwanamke anayetaka tu ku-date. Lakini, kama unahitaji mahusiano ambayo yapo serious, pambana kuwa imara na mwenye kujiweza kimaisha.[Soma: Nini wanaume hufikiri kinawavutia wanawake na ni nini hasa huwavutia wanawake!]

Kwa pande mwingine kama upo na msichana na unataka kubadilisha uhusiano wenu, inatakiwa ubadilike ufanye yale yote mwanaume wake a baadaye anataka aweje.

Simaanishi uyaache maisha yako na uanze kuigiza - Hapana. Ila unataka kubadili mtazamo wako kwenye mahusiano na kwa wanawake pia, na sasa unaangalia kitu ambacho unaweza kuvuna kutoka katika uhusiano huo. Kama uataka ku-date kawaida, na matendo yako yanasema unataka uhusiano serious, unaweza ukawa na maendeleo katika mtazamo wa kimahusiano. Lakini point ni kwamba jaribu na jitahidi sana kuyaoangilia matendo yako na matamanio yako.

[Soma: Mambo 25 yanayomfanya mwanaume asiwe na kipingamizi kwa mwanamke!]

Mwisho wa siku, kuwa mwanaume anayetaka ku-date nae au kuwa mwanaume anayetamani umuoe haikufanyi wewe kuwa mtu wa tofauti. Ni mitazamo tofauti na malengo tofauti katika hatua fulani kwenye maisha. Utu wako bado utabaki palepale, na utabaki kuwa vile vile licha ya hayo yote.
Kama imekufungua na imekusaidia kujibu maswali mengi uliyokuwa ukijiuliza basi share na mwenzako ili imsaidie kama ilivyokusaidia wewe.

0 Response to "Mwanaume na Mwanamke wanaotaka 'kutoka' wote V.s Mwanaume na Mwanamke wanaotaka kuoana!"

Post a Comment