MNAOSEMA VYA KALE NI DHAHABU - Bongo Loves

MNAOSEMA VYA KALE NI DHAHABU


MNAOPENDA KURUDIA YA ZAMANI ETI NI DHAHABU
Leo nazungumza na WANAUME/WANAWAKE wanaohitaji kurudiana na wapenzi, waume au wake zao💘
Kwanza kabisa niwakumbushe kwamba KUSHINDWA KUUTUNZA UPENDO WA AWALI MNAKUTANA NI SAWA NA KUCHIMBA SHIMO NA UTELEZE UDUMBUKIE MWENYEWE😂😂
Mapenzi ni UTASHI na kwa namna yoyote ile UTASHI ndo hujenga SHAUKU YA UHITAJI... Wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoea kwamba bila fulani siwezi kuendelea, badala ya kusimamia misingi ya UPENDO unaendekeza mazoea mwisho wako lazima uwe mbaya tu😭
Ni kweli MAZOEA nayo ni kama kachumbari kwenye MAHUSIANO lakini mazoea hayo hayo YAMEHARIBU MAHUSIANO MENGI! Huwezi kuanza kutafuta watu "VIKAO" kunusuru PENZI lako, Kwani kwa uhalisia mlikutana wawili na kila mmoja akawa na mhemko na mwenzie iweje mshindwe kufikia maridhiano hata mkatoka kwenye usiri wa penzi lenu na kuanza kutafuta mshenga🤷🏽‍♂
Mshenga hawezi kunusuru NDOA⛔
Wazazi hawawezi kuwa suruhu ya matatizo yenu, Shekhe, Mchungaji wanabaki kuwa walibariki ndoa yenu tu, Utaliwa pesa na waganga kutafuta Mwenza wako akurudie, Rejea kwenye misingi ya UPENDO 💘
Zikumbuke zile nyakati mwenza wako alikuwa MDHAIFU KWAKO Kwani ulifanyaje mpaka akajikuta ni mdhaifu kwako🤷🏽‍♂
Ni mambo yapi ulikuwa ukitekeleza kwake hata akawa anafurahia uwepo wako kwake?
Ni kipi ulifanya ama kuonyesha hata akajikuta ni mwenye FURAHA💃 NA AMANI✌🏼
Huna haja ya kusumbuka kutanga na njia kutafuta suruhu ya PENZI lako wakati huwezi kukumbuka MLIANZAJE HUKO MWANZO👫
Upendo unatokana na uhitaji kwa mazingira husika, Kama mtu ameishi nawe na kubaini kwamba HUMPENDI TENA automatically MOYO wake unafubaa na kukosa sababu ya kuendelea, Watu mmejikuta mnambebesha MUNGU lawama juu ya mambo ambayo yapo kwenye uwezo wa ki bin adam, Unamfuata Mtu akusaidie namna ya kurudiana na mke/mume wako wakati yeye mwenyewe NDOA YAKE INAFUKUTA kama haijafa kabisaaa😂😂
Huwezi kumrejesha MPENZI, MUME AU MKE wako kwa kutorejea kwenye chanzo cha tatizo na ukaweka TUMAINI kwake ya kwamba hutamuumiza tena, Matendo ya mabadiliko ya tabia iliyomuudhi mwenza wako ni suruhu njema sana kumpa mafikirio mema mwenza wako juu yako, Kwanza lijue tatizo lililoboa PENZI lenu ili uweze kujitafakari na kujipa muda wa KUPANGA NAMNA NZURI YA KUMREJESHA MWENZA WAKO💪🏽
Mbinu, Ubunifu, Muda, Uaminifu pamoja na lugha nzuri nadhani hizo ndizo zilijenga DHAMANA moyoni mwake IWEJE LEO HUWEZI KUSIMAMIA HAYO?
Mchawi wa penzi lako ni UBABE, UPUUZAJI, DHARAU na Mengine yanayofanana na hayo, Ni Mchungaji/Shekhe gani ataingia akilini mwako kwenda kuzuia
HASIRA ILIYOPELEKEA UGOMVI WENU?
MAPENZI ni ya wawili walioamua kuunganisha umoja wao kupitia UPENDO sasa kama wewe huna viashiria vya UPENDO kwa mwenza wako TARAJIA KUMPA MASWALI NA MAWAZO MENGI lakini naomba nikwambie "USIPOGUNDUA MAPEMA KWAMBA PENZI LAKO LIPO UKINGONI BASI HUWEZI PIA KULINUSURU maana wewe mwenyewe hujui kujipigania"

0 Response to "MNAOSEMA VYA KALE NI DHAHABU"

Post a Comment